Kuomboleza na taazia

Tuandikie

• Ni sunna kuomboleza watu waliofiwa kwa kusema, ((Inna lilaahi maa akhadha walahu ma A’atwa, wakulu shay-in ‘indahu bi ajali musammaa, faswbir wahtasib)). Hii dua imethibiti kutoka kwa Mtume صلي الله عليه وآله وسلم Muttafaqun ’alayhi. Maana ya dua hii ni (hapana shaka ni chake Mwenyezi Mungu alichokitwaa na ni chake alichokitoa, na kila jambo kwake ni kwa wakati na muda maalum (uliopangwa), basi fanya subira na utaraji malipo) na vile vile Mtume صلي الله عليه وآله وسلم akisema, ((Mwenyezi Mungu azidishe ujira wako)) au ((Mwenyezi mungu aufanye bora msiba wako)).

• Inaruhusiwa kulia katika msiba bila kuvuka mipaka, kwani Mtume صلي الله عليه وآله وسلم alilia alipofiwa na mwanawe Ibrahim. Mutafaqun ’alayh. Na kulia kwenyewe kusiwe kwa mayowe na NADAB (kulia na huku unataja sifa na mazuri ya marehemu).

• Inafaa kwa mfiwa kuomboleza maiti yake, yaani aache biashara yake au safari zisizokuwa na lazima n.k. Na kuomboleza kwenyewe kuwa kwa siku tatu tu isizidi, ila kwa mke aliyefiwa na mumewe, yeye ataomboleza kwa muda wa EDA yake yaaani miezi minne na siku kumi, na akiwa ni mwenye mimba basi hadi atakapojifungua.

• Ni haramu kabisa NADAB na NIYAAHA juu ya maiti, NADAB ni kutaja mazuri ya maiti na kuyahesabu, na NIYAAHA ni kulia kwa kupiga mayowe na huku akiongea vitu tofauti kuhusu maiti na kutoa sauti ya ajabu. Hakika kufanya hivyo ni kupingana na QADAR (Mipango ya Mwenyezi Mungu).

 

[Utangulizi] [Kumuosha maiti] [Kumkafini maiti] [Swala ya jenaza] [Kubeba jenaza na kuzika] [Kuomboleza na taazia]